Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kuongeza masoko ya kubadilisha fedha ya Ethereum

Mtu yeyote yuko huru kupendekeza masoko mapya ya kubadilisha fedha kwenye ethereum.org.

Kwa sasa tunayaorodhesha kwenye:

Ukurasa huu unamruhusu mtumiaji kuweka mahali anapoishi na kuona ni masoko gani ya kubadilisha fedha anayoweza kutumia. Hii inasaidia kuonyesha vizuizi vyovyote vya kijiografia mapema.

Kwa sababu ya muktadha huu, tunahitaji maelezo fulani mahususi unapopendekeza soko la kubadilisha fedha.

KUMBUKA: Ikiwa unataka kuorodhesha soko lililogatuliwa la kubadilisha fedha, angalia sera yetu ya kuorodhesha pochi na programu tumizi zilizogatuliwa (dapps).

Tunachohitaji

  • Vizuizi vya kijiografia vinavyotumika kwenye soko la kubadilisha fedha. Vizuizi vya kijiografia vinavyohusishwa na soko la kubadilisha fedha vinapaswa kufafanuliwa kwenye ukurasa maalum au sehemu ya tovuti ya soko hilo.
  • Fedha ambazo watumiaji wanaweza kutumia kununua ETH
  • Uthibitisho kwamba soko la kubadilisha fedha ni kampuni halali ya biashara
  • Maelezo yoyote ya ziada ambayo unaweza kuwa nayo – haya yanaweza kuwa maelezo kuhusu kampuni kama vile miaka ya kufanya kazi, ufadhili wa kifedha n.k.

Tunahitaji maelezo haya ili tuweze kwa usahihi kuwasaidia watumiaji kupata soko la kubadilisha fedha wanaloweza kutumia.

Na ili ethereum.org iweze kuwa na uhakika zaidi kwamba soko la kubadilisha fedha ni huduma halali na salama.


Ongeza soko lako la kubadilisha fedha

Ikiwa unataka kuongeza soko la kubadilisha fedha kwenye ethereum.org, tengeneza suala kwenye GitHub.

Tengeneza suala (opens in a new tab)

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 6 Juni 2026