Hatuwezi kutarajia kuangazia kila kitu kuhusu Ethereum kwa hivyo tunajaribu kuonyesha baadhi ya makala bora, mafunzo, majarida, bodi za kazi na rasilimali mbalimbali za maudhui ambazo jamii inaunda. Hizi mara nyingi hutoa maelezo ya kina zaidi kuhusu mada ambazo watumiaji wanaweza kuvutiwa nazo.
Ikiwa kuna rasilimali ya maudhui ambayo unahisi inapaswa kuongezwa kwenye ukurasa, jisikie huru kuipendekeza mahali panapofaa.
Jinsi tunavyoamua
Rasilimali za kujifunza zitatathminiwa kwa vigezo vifuatavyo:
- Je, maudhui yamesasishwa?
- Je, maudhui yanahitaji malipo ili kufikiwa?
- Je, taarifa ni sahihi? Je, inategemea ukweli au maoni?
- Je, mwandishi anaaminika? Je, wanarejelea vyanzo vyao?
- Je, maudhui haya yanaongeza thamani tofauti ambayo rasilimali/viungo vilivyopo haviangazii?
- Je, maudhui haya yanahudumia mojawapo ya aina za watumiaji (opens in a new tab) wetu?
Ongeza rasilimali yako ya maudhui
Ikiwa unataka kuongeza rasilimali ya maudhui kwenye ethereum.org na inakidhi vigezo, tengeneza ishu kwenye GitHub.
Tengeneza ishu (opens in a new tab)