Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 15 Agosti 2023

Dhamira na maono

Jamii ya Ethereu inalenga kuwa ya ulimwengu wote na inayojumuisha, japo maudhui yake yanahudumia wazungumzaji wa kiingereza tu, na ikiacha watu bilioni 6 wasiozungumza kiingereza. Ili Ethereum.org ifanye kazi kama lango la Ethereum kwa jamii duniani kote, tunaamini kutoa maudhui ya Ethereum kwa wasiozungumza kiingereza katika lugha zao ni kitu muhimu.

Programu ya Ufasiri wa ethereum.org unalenga kuifanya Ethereum kupatikana kwa kila mmoja kwa kufasiri ethereum.org na maudhui mengine ya Ethereum kwenda katika lugha nyingi iwezekanavyo.

Dhamira yetu

  • Kuto matoleo yaliotafsiriwa ya tovuti kuwawezweha wageni duniani kote kujifunza kuhusu Ethereum kwenye lugha zao za asili
  • Wezesha ujio wa wanachama zaidi kwenye jumuiya ya kimataifa ya Ethereum
  • Ruhusu kushiriki kwa urahisi zaidi na kujumuisha zaidi taarifa na maarifa ya Ethereum
  • Wawezeshe wanajamii kuchangia tafsiri kwa Ethereum na kuweka alama zao kwenye mfumo wa ikolojia
  • Tambua, ungana na, na utoe mwongozo kwa wachangiaji wenye shauku wanaotaka kujihusisha na mfumo ikolojia

Maono yetu

  • Tafsiri maudhui muhimu kwa wanachama wa jumuiya ya Ethereum kutoka nchi na sehemu nyingi za dunia iwezekanavyo
  • Kuunga mkono ugawanaji wa maarifa katika lugha mbalimbali ili kuunda jamii ya Ethereum iliyo na habari bora na iliyoelimika
  • Kuongeza ushirikishwaji na ufikiaji wa Ethereum kwa kuondoa vizuizi vya lugha vinavyowazuia wasiozungumza Kiingereza kujiunga na mfumo wa ikolojia

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 15 Agosti 2023

Je! makala haya yamekusaidia?