Muundo wa data na usimbuaji
Ukurasa ulihaririwa mwisho: 15 Agosti 2023
Ethereum hutengeneza, huhifadhi na huhamisha idadi kubwa ya data. Data hii lazima iumbizwe kwa njia sanifu na zenye ufanisi wa kumbukumbu ili kumruhusu yeyote kuendesha nodi kwenye maunzi ya kiwango cha watumiaji ya kawaida. Ili kufanikisha hili, miundo kadhaa maalum ya data hutumika kwenye mkusanyiko wa Ethereum.
Mahitaji ya awali
Unapaswa kuelewa misingi ya Ethereum na programu za wateja. Ufahamu wa safu ya mtandao na Karatasi nyeeupe ya Ethereum unapendekezwa.
Miundo ya data
Patricia merkle tries
Patricia Merkle Tries ni miundo ambayo huweka msimbo jozi za thamani muhimu katika trie iliyothibitishwa kwa njia fiche na ya uhakika. Hizi hutumiwa sana katika safu ya utekelezaji ya Ethereum.
Zaidi kuhusu Patricia Merkle Tries
Kiambishi awali cha urefu kinachojirudia
Kiambishi awali cha urefu kinachojirudia (RLP) ni mbinu ya uratibishaji inayotumika sana katika safu ya utekelezaji ya Ethereum.
Uratibishaji Rahisi
Uratibishaji Rahisi (SSZ) ndiyo muundo mkuu wa uratibishaji kwenye safu ya makubaliano ya Ethereum kwa sababu ya uoanifu wake na uwekaji wa merkle.