Ruka kwenda kwenye maudhui makuu
Change page

Kupeleka mikataba erevu

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 17 Desemba 2025

Unahitaji kupeleka mkataba wako-erevu ili uweze kupatikana kwa watumiaji wa mtandao wa Ethereum.

Ili kupeleka mkataba-erevu, unahitaji tu kutuma muamala wa Ethereum wenye msimbo ulioandaliwa wa mkataba-erevu bila kubainisha mpokeaji yeyote.

Mahitaji ya awali

Unapaswa kuelewa mitandao ya Ethereum, miamala na muundo wa mikataba-erevu kabla ya kupeleka mikataba-erevu.

Kupeleka mkataba pia hugharimu ether (ETH) kwa kuwa huhifadhiwa kwenye mnyororo wa bloku, kwa hivyo unapaswa kufahamu gesi na ada kwenye Ethereum.

Mwisho, utahitaji kuandaa mkataba wako kabla ya kuuwasilisha, kwa hiyo hakikisha umesoma kuhusu kuandaa mikataba-erevu.

Jinsi ya kupeleka mkataba-erevu

Vitu utakavyohitaji

  • Bytecode ya mkataba wako – hii hutengenezwa kupitia uandaaji
  • ETH ya gesi – utaweka kikomo chako cha gesi kama miamala mingine kwa hiyo fahamu kwamba upelekaji wa mkataba unahitaji gesi nyingi zaidi kuliko uhamisho rahisi wa ETH
  • hati ya upelekaji au programu-jalizi
  • ufikiaji wa nodi ya Ethereum, ama kwa kuendesha yako mwenyewe, kuunganisha kwenye nodi ya umma, au kupitia ufunguo wa API kwa kutumia huduma ya nodi

Hatua za kupeleka mkataba-erevu

Hatua mahususi zinazohusika zitatategemea mfumo wa usanidi unaohusika. Kwa mfano, unaweza kuangalia nyaraka za Hardhat kuhusu kupeleka mikataba yako (opens in a new tab) au nyaraka za Foundry kuhusu kupeleka na kuthibitisha mkataba-erevu (opens in a new tab). Mara tu utakapowasilishwa, mkataba wako utakuwa na anwani ya Ethereum kama akaunti zingine na unaweza kuthibitishwa kwa kutumia zana za uthibitishaji wa msimbo chanzo.

Remix - Remix IDE huruhusu kusanidi, kupeleka na kusimamia mikataba-erevu kwa minyororo ya bloku kama Ethereum

Tenderly - Jukwaa la usanidi la Web3 ambalo hutoa utatuzi, uangalizi, na vizuizi vya ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya kusanidi, kujaribu, kufuatilia na kuendesha mikataba-erevu

Hardhat - Mazingira ya usanidi ya kuandaa, kupeleka, kujaribu na kutatua programu yako ya Ethereum

thirdweb - Peleka mkataba wowote kwa urahisi kwenye mnyororo wowote unaoendana na EVM, kwa kutumia amri moja

Crossmint - Jukwaa la usanidi la web3 la kiwango cha biashara la kupeleka mikataba-erevu, kuwezesha malipo ya kadi za mkopo na mnyororo-mbali, na kutumia API kuunda, kusambaza, kuuza, kuhifadhi na kuhariri NFTs.

Masomo zaidi

Unajua rasilimali ya jamii iliyokusaidia? Hariri ukurasa huu na uiongeze!_

Je! makala haya yamekusaidia?