Utangulizi wa kiufundi wa Ether
Ukurasa ulihaririwa mwisho: 7 Agosti 2025
Mahitaji ya awali
Ili kukusaidia kuelewa ukurasa huu vizuri, tunapendekeza usome kwanza Utangulizi wa Ethereum.
Sarafu ya Kripto ni nini?
Sarafu ya kripto ni njia ya mabadilishano inayolindwa na leja ya msingi wa mnyororo wa bloku.
Njia ya mabadilishano ni kitu chochote kinacho kubaliwa na wengi kama malipo ya bidhaa na huduma na leja ni uhifadhi wa data ambao hufatilia miamala. Teknolojia ya mnyororo wa bloku inaruhusu watumiaji kufanya miamala klatika leja bila kutegemea mtu wa tatu anaye aminika kutunza leja.
Sarafu ya kwanza ya kidijitali ilikuwa Bitcoin, iliyoundwa na Satoshi Nakamoto. Tangu kuanzishwa kwa Bitcoin mnamo mwaka 2009, watu wametengeneza maelfu ya sarafu za kidijitali katika minyororo wa bloku mbalimbali.
Ether ni nini?
Ether (ETH) ni sarafu ya kidigitali inayotumika kwa mambo mengi kwenye mtandao wa Ethereum. Kimsingi, ndiyo njia pekee inayokubalika ya malipo kwa ada za miamala, na baada ya The Merge, ether inahitajika ili kuthibitisha na kupendekeza vizuizi kwenye Mainnet. Ether pia hutumika kama aina ya msingi ya dhamana katika masoko ya ukopeshaji ya DeFi, kama kipimo cha hesabu katika masoko ya NFT, kama malipo yanayopatikana kwa kutoa huduma au kuuza bidhaa halisi za ulimwengu, na zaidi.
Ethereum inaruhusu wasanidi programu kuunda mfumo uliotawanywa (mfumo mtawanyo wa kimamlaka), ambapo zote hushiriki bwawa la nguvu za kompyuta. Bwawa hili ni ndogo, hivyo Ethereum inahitaji utaratibu wa kuamua ni nani atakayelipata kulitumia. Vinginevyo, mfumo mtawanyo wa kimamlaka unaweza kwa bahati mbaya au kwa nia mbaya kutumia rasilimali zote za mtandao, jambo ambalo lingezuia wengine kuufikia.
Sarafu ya kidigitali ya ether inasaidia utaratibu wa bei kwa nguvu za kompyuta za Ethereum. Watumiaji wanapotaka kufanya muamala, lazima walipe ether ili muamala wao utambuliwe kwenye mnyororo wa vizuizi. Gharama hizi za matumizi zinajulikana kama ada za gesi, na ada ya gesi inategemea kiasi cha nguvu ya kompyuta inayohitajika kutekeleza muamala na mahitaji ya mtandao mzima ya nguvu ya kompyuta kwa wakati huo.
Kwa hivyo, hata kama mfumo mtawanyo wa kimamlaka wenye nia mbaya ungewasilisha kitanzi kisicho na kikomo, hatimaye muamala ungeishiwa na ether na kukoma, na kuruhusu mtandao kurudi katika hali ya kawaida.
Ni kawaida kuchanganyaopens in a new tab Ethereum na ether — watu wanaporejelea "bei ya Ethereum," wanakuwa wanaelezea bei ya ether.
Kutengeneza ether
Kutengeneza ni mchakato ambapo ether mpya huundwa kwenye leja ya Ethereum. Itifaki ya msingi ya Ethereum huunda ether mpya, na haiwezekani kwa mtumiaji kuunda ether.
Ether hutengenezwa kama zawadi kwa kila kizuizi kinachopendekezwa na katika kila kituo cha ukaguzi cha epoch kwa shughuli zingine za mthibitishaji zinazohusiana na kufikia makubaliano. Jumla ya kiasi kilichotolewa inategemea idadi ya wathibitishaji na kiasi cha ether walichoweka kama hisa. Jumla ya utoaji huu umegawanywa kwa usawa miongoni mwa wathibitishaji katika hali bora ambapo wathibitishaji wote ni waaminifu na wako mtandaoni, lakini katika hali halisi, hutofautiana kulingana na utendaji wa mthibitishaji. Takriban 1/8 ya jumla ya utoaji huenda kwa mpendekezaji wa kizuizi; salio husambazwa kwa wathibitishaji wengine. Wapendekezaji wa vizuizi pia hupokea vidokezo kutoka kwa ada za miamala na mapato yanayohusiana na MEV, lakini hizi hutoka kwa ether iliyorejelezwa, si utoaji mpya.
Kuchoma ether
Pamoja na kuunda ether kupitia zawadi za vizuizi, ether inaweza kuharibiwa kupitia mchakato unaoitwa 'kuchoma'. Wakati ether inapochomwa, huondolewa kwenye mzunguko kabisa.
Uchomaji wa Ether hutokea katika kila muamala kwenye Ethereum. Watumiaji wanapolipa miamala yao, ada ya msingi ya gesi, iliyowekwa na mtandao kulingana na mahitaji ya miamala, huharibiwa. Hii, pamoja na ukubwa wa vizuizi unaobadilika na ada ya juu zaidi ya gesi, hurahisisha ukadiriaji wa ada ya muamala kwenye Ethereum. Mahitaji ya mtandao yanapokuwa juu, vizuiziopens in a new tab vinaweza kuchoma ether nyingi kuliko wanavyotengeneza, na hivyo kusawazisha utoaji wa ether.
Kuchoma ada ya msingi kunazuia uwezo wa mzalishaji wa kizuizi kuchezea miamala. Kwa mfano, kama wazalishaji wa vizuizi wangepokea ada ya msingi, wangeweza kujumuisha miamala yao bila malipo na kuongeza ada ya msingi kwa kila mtu mwingine. Vinginevyo, wangeweza kurejesha ada ya msingi kwa baadhi ya watumiaji nje ya mnyororo, na kusababisha soko la ada ya miamala lisilo wazi na gumu zaidi.
Madhehebu ya ether
Kwa kuwa thamani ya miamala mingi kwenye Ethereum ni ndogo, ether ina madhehebu kadhaa ambayo yanaweza kurejelewa kama vipimo vidogo vya hesabu. Kati ya madhehebu haya, Wei na gwei ni muhimu hasa.
Wei ni kiasi kidogo zaidi cha ether kinachowezekana, na matokeo yake, utekelezaji mwingi wa kiufundi, kama vile Karatasi ya Njano ya Ethereumopens in a new tab, utategemea mahesabu yote katika Wei.
Gwei, kifupi cha giga-wei, hutumiwa mara kwa mara kuelezea gharama za gesi kwenye Ethereum.
| Dhehebu | Thamani katika ether | Matumizi ya Kawaida |
|---|---|---|
| Wei | 10-18 | Utekelezaji wa kiufundi |
| Gwei | 10-9 | Ada za gesi zinazoweza kusomwa na binadamu |
Kuhamisha ether
Kila muamala kwenye Ethereum una sehemu ya value, ambayo hubainisha kiasi cha ether kitakachohamishwa, kilichoonyeshwa kwa wei, kutumwa kutoka kwa anwani ya mtumaji hadi anwani ya mpokeaji.
Wakati anwani ya mpokeaji ni mkataba mahiri, ether hii iliyohamishwa inaweza kutumika kulipia gesi wakati mkataba mahiri unapotekeleza msimbo wake.
Kuuliza kuhusu ether
Watumiaji wanaweza kuuliza kuhusu salio la ether la akaunti yoyote kwa kukagua sehemu ya balance ya akaunti, ambayo huonyesha umiliki wa ether ulioonyeshwa kwa wei.
Etherscanopens in a new tab na Blockscoutopens in a new tab ni zana maarufu za kukagua salio za anwani kupitia programu za wavuti. Kwa mfano, ukurasa huu wa Blockscoutopens in a new tab unaonyesha salio la Wakfu wa Ethereum. Salio za akaunti pia zinaweza kuhojiwa kwa kutumia mikoba au moja kwa moja kwa kufanya maombi kwa nodi.
Masomo zaidi
- Kufafanua ether na Ethereumopens in a new tab – Kundi la CME
- Karatasi Nyeupe ya Ethereum: Pendekezo la asili la Ethereum. Hati hii inajumuisha maelezo ya ether na motisha nyuma ya uundaji wake.
- Kikokotoo cha Gweiopens in a new tab: Tumia kikokotoo hiki cha gwei kubadilisha wei, gwei na ether kwa urahisi. Weka tu kiasi chochote cha wei, gwei, au ETH na uhesabu ubadilishaji kiotomatiki.
Unajua rasilimali ya jamii iliyokusaidia? Hariri ukurasa huu na uiongeze!_